Thursday, June 21, 2012

Mambo wa kusafisha maji chumvi - water desalination plant


Zanzibar ni nchi ambayo inaanza kukabiliwa na uhaba wa maji kutokana na sababu tofauti, zikiwemo uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la watumiaji yakiwemo mahoteli ya kitalii.

Ni vyema serikali ikaanza na mapema kueka mkakati wa kukabiliana na uhaba wa maji, ikiwemo mbinu hii moja ambayo nchi zilizoendelea na zilizo na fedha zimeanza kutumia nayo ni kubadilisha maji ya bahari kuweza kutumika kwa matumizi ya mwanadamu.

Si haba tumezungumkwa na bahari, kinachohitajika ni mipango ya mapema ya hapo baadaye kuwa na mitambo ya kusafisha maji ya bahari. Tuanze mipango hiyo sasa.

No comments:

Post a Comment